Gavana wa jimbo la Kivu Kusini aombwa kupunguza beyi yakushiriki kwenye mitihani zaki serkali.
Published on Friday 06 May 2022 - 15:55
Mzalendo Grégoire Lapenzi aomba kupunguzwa kwa bei ya ada ya ushiriki wa mtihani wa mwaka wa 2022.
Alitoa ombi hili muchana ya Ijumaa hii, Mei 6, 2022 wakati wa mahojiano yaliyotolewa kwa media actualiteuvira.net katika jiji la Uvira nchini DRC, jimboni Kivu ya Kusini.
Kulingana na Mzalendo Grégoire Lapenzi, hali ya maisha ya wakazi wa Kivu Kusini inazidi kuwa mbaya kufuatia visa vingi vya mafuriko, majanga ya asili, ukosefu wa usalama na watu wengi kuyahama makazi yao eneo kuliko sababishwa na migogoro.
Akikabiliwa na mazingira haya, mzalendo Grégoire Lapenzi anamwomba gavana wa Kivu Kusini kufuta agizo la kuweka ada za kushiriki katika mitihani ya serikali kwa dola 47 ili kuweka ada hizi kuwa dola 25 za Kimarekani.
« Tunajutia kinachoendelea katika nchi yetu, hali ya maisha ya wananchi ni mbaya, lakini mamlaka zetu zinapandisha bei ya ada za shule. Mamlaka ya mkoa lazima iwe na huruma kwa idadi ya watu wake. Ni lazima ikague bei kwa kuweka gharama hizi kwa dola 25 katika jimbo lote la Kivu Kusini. » aliomba hivo Mzalendo Grégoire Lapenzi.
Alifahamisha kuwa wananchi wanaoishi katika nyanda za juu na kati za Uvira, Fizi na Mwenga hawataweza kulipa dola 47, achilia mbali dola 25, kutokana na majanga wanayopitia katika eneo hili la kusini mwa jimbo la Kivu Kusini linalokumbwa na ukosefu wa usalama unaoongezeka.
Mzalendo Grégoire Lapenzi anadhani kwamba serikali inapaswa kugharamia ushiriki wa EXETAT kwa watu hawa ili kuwanusuru, kwa kuzingatia hali ambayo wamekuwa wakipitia kwa miaka kadhaa. Hii ndiyo sababu mpatanishi wetu anamwomba Gavana Théo Ngwabidje kuwa na huruma, nakusamehe gharama hizi kwa wakazi wa maeneo haya matatu hadi kiasi hicho kitakapowekwa kuwa dola 15.
Mzalendo Grégoire Lapenzi anawaalika wabunge wa majimbo kujihusisha zaidi ili ada hizi zishushwe kwa kiwango kinachokubalika kulingana na hitaji za watu.
Uandishi.
Les Articles Recents
Publié le 04/02/2026 - 09:29
Publié le 03/02/2026 - 18:50
Uvira : MICHE-asbl forme des femmes leaders communautaires sur la paix et la cohésion sociale.
Publié le 03/02/2026 - 17:52
Publié le 29/01/2026 - 21:54
Publié le 29/01/2026 - 21:35
